Header Ads

Header Ads

MCHUNGAJI ALIEBAKWA SIKU YAKE YA HARUSI NA KUHARIBIWA KIZAZI NA KUAMUA KUWASAMEHE JE NINI KILIMTOKEA TENA SOMA HAPA!!


“Nimewasamehe washambuliaji wangu,” mchungaji Terry Gobanga wa Kenya aliiambia BBC. “Haikuwa rahisi lakini Imani yangu pia inanihimiza kusamehe na si kulipa mabaya kwa uovu lakini kwa wema.”
Miaka michache iliyopita, Gobanga alikuwa anatarajia kujiandaa kufunga ndoa yake na mchumba wake Harry, katika Kanisa la All Saints Cathedral huko Nairobi, ambapo waumini wote wa kanisa hilo na familia yake ilikuwa huko.
Hata hivyo, alichotegemea kuwa siku hiyo itakuwa ya furaha zaidi katika maisha yake ikageuka kuwa ndoto yenye machungu na masikitiko makubwa.
Siku ya harusi yake, alipokuwa akitembea kwenda nyumbani kutoka kwenye kituo cha basi, Gobanga alitekwa ghafla na kuingizwa kwenye gari na watu wasiojulikana, wakamtupa kwenye kiti cha nyuma ya gari na yote hayo yalitokea ndani ya sekunde chache,” alikumbuka.
“Kipande cha kitambaa kilifungwa kwenye kinywa changu nilikuwa nikihangaika sana huku nikikataa na kujaribu kupiga kelele. Nilipofanikiwa kutoa kile kitambaa, nilipiga kelele: ‘Leo ni siku yangu ya harusi!’ Hapo ndipo nilipopata pigo la kwanza kutoka kwa mmoja wa wanaume aliniambia ‘tushirikiane au la utakufa’. ”
Mchungaji Terry Gobanga.
Gobanga aliiambia BBC kuwa wanaume hao walipokezana zamu kumbaka.
“Nilihisi kuwa nitakufa,” Gobanga alikiri. “Nilikuwa bado napigana kwa ajili ya maisha yangu, hivyo wakati mmoja wa wanaume aliyefanikiwa kunitoa kile kitambaa kinywani mwangu nilimchoma na viatu vyangu nilivyovaa alilia kwa uchungu na mmoja wao alinipiga tumboni. Hapo ndipo walipofungua mlango na kunitupa nje ya gari.
Mwanamke huyo hatimaye aliokolewa baada ya mtoto mmoja kumwona akitupwa kutoka kwenye gari na akamwita bibi yake, ambaye aliwaita polisi. Walimchukua na walidhani alikuwa amekufa, wakati wanampeleka mochwari njiani alianza kukohoa na hapo ndipo walipoamua kumpeleka hospitali.
“Nilikuwa nusu uchi nikiwa nimetapakaa damu, na uso wangu ulikuwa umevimba kutokana na kuadhibiwa,” alisema. “Lakini kuna kitu kilichomstua muuguzi mmoja kuhusu mimi kutokana na kupata taarifa za kupotea kwa  bibi harusi katika moja ya makanisa yaliyopo mjini pale.. na akasema ‘Hebu tuzunguke makanisa yote ya mahali hapa ili kuona kama kuna bibi harusi yeyote aliyepotea,’ aliwaambia wauguzi.”
Baada ya kusambaa kwa taarifa juu ya tukio hilo wazazi wake na mchumba wake walikwenda hospitali na wageni wote.
Alipokuwa hospitalini, Gobanga alifahamishwa kuwa hawezi kuwa na watoto tena kutokana na vile alivyopigwa tumboni. Alisikitika sana, na aliomba sana msamaha kwa mchumba wake Harry kwa yaliyotokea.
“Watu wengi walikuwa wakinilaumu kwa kile kilichotokea hakika iliniumiza sana, lakini familia yangu na mchumba  wangu Harry waliniunga mkono,” alisema.
Terry akimvisha pete ya ndoa mume wake Harry(ambaye kwasasa ni marehemu).
Wanandoa hao waliweza kuandaa harusi nyingine, ambayo ilifanyika Julai 2005. Hata hivyo, siku 29 tu baadaye, Harry alikufa kwa moshi weye sumu ya kaboni ya monoxide baada ya ajali iliyotokana na uchomaji wa mkaa.
“Kurudi kanisani kwa ajili ya mazishi ilikuwa ni hali ya kutisha sana kwangu,” alisema Gobanga. “Mwezi mmoja nyuma nilikuwa pale katika mavazi yangu meupe, na mume wangu Harry akisimama mbele akiwa mtanashati sana ndani ya suti yake na sasa, nilikuwa nimevaa mavazi ya rangi nyeusi na Harry alikuwa akisukumwa katika jeneza.”
Matukio hayo mabaya yalimfanya mwanamke huyu kuhoji imani yake: “Nilihisi nimepewa adhabu na Mungu, nilihisi nimedharauliwa na kila mtu .. Sikuamini kwamba watu wanaweza kucheka, kwenda nje na kuendelea na maisha yao tu.
“Siku moja nilikuwa nimekaa kwenye kiti nikitazama ndege huku nikisema: ‘Mungu, unawezaje kuwatunza ndege na sio mimi?’ papo hapo nikakumbuka kuwa kuna masaa 24 kwa siku – kukaa katika msongo wa mawazo na mapazia yako yakiwa yamefungwa, hakuna mtu atakayekurudishia nyuma saa hizo 24. Kabla ya kujua, ni wiki, miezi, miaka mingapi iliyopotea. kwakweli inauzima sana. ”
Mchungaji Terry akiwa na mume wake Tony Gobanga.
Mungu alikuwa na mpango bora zaidi wa maisha yake, Hatimaye, baadae alipendana na rafiki, Tony Gobanga, na hao wawili waliamua kuoana.
“Ilikuwa miaka mitatu baada ya ndoa yangu ya kwanza, na niliogopa sana. Tulipokuwa tukibadilishana ahadi, nilifikiri: ‘Hapa mimi ni Baba tena, tafadhali usiruhusu afe.’ Wakati kutaniko lilipomwombea nililia bila kusubiri. ”
Mchungaji Terry Gobanga akiwa na familia yake.
Kwa uwezo wa ajabu, Gobanga alipata ujauzito mwaka mmoja baadaye, na leo, wanandoa hawa wana binti wawili Tehille na Towdah. Gobanga ameandika hadithi yake hii ya ushuhuda katika kitabu, kiitwacho Crawling out of Darkness (Kutoka nje ya giza), na pia ameanzisha shirika ambalo linatoa ushauri na msaada kwa waathirika wa ubakaji.

No comments: